Ruto ana mpango gani baada ya Mariga kutemwa nje kwenye kinyang’anyiro cha Kibra?

Image result for mariga and ruto

Kinyang’anyiro cha kiti cha Kibra kimezua utata na kwa sasa Jubilee inaonekana kupoteza mwelekeo baada ya McDonald Mariga kuondolewa.

Naibu Rais William Ruto ambaye amekuwa kipaumbele kwenye kampeni za Mariga bado hajatoa kauli yake kuhusu IEBC ya Kibra kutangaza kuwa Mariga sio mpiga kura.

Kulingana na kifungu cha 5 (1) b cha Sheria ya Uchaguzi, shughuli zote za uchaguzi pamoja na usajili wa wapiga kura lazima zisitishe baada ya kutangaza nafasi.

“Mariga aliomba usajili mnamo Agosti 26 baada ya kutangazwa kwa nafasi hiyo mnamo Agosti 14 na IEBC ikatangaza uchaguzi mdogo mnamo Agosti 16, siku mbili baadaye. Kwa sheria, maombi lazima yaletwe makao makuu na maelezo yote yaliyothibitishwa kabla ya kuwekwa kwenye safu ya wapiga kura. Mara tu hiyo ikifanyika rejista italazimishwa kutangazwa,” Afisa wa IEBC alielezea.

Muli ambaye ni afisa wa IEBC Kibra alikataa kumpitisha Mariga kwani alihofia atashutumiwa binafsi kwa kuendeleza uhalifu wa uchaguzi.

Mariga ana siku saba sasa kukata rufaa kama bado anataka kuwa kwenye debe hilo la Novemba 7 akimenyana na Owalo wa ANC, Imran OKoth wa ODM na wengine wengi.

Lakini je, Mariga atasubiri mwaka wa 2022 ili kuwania kiti hicho baada ya kutatua shida alizo nazo ama Hustler mwenyewe naibu rais ataingilia kati na kumregesha kwenye debe?

 

Do you have any information that you would like Daily Buzz to publish or highlight? Get to us on info@dailybuzz.co.ke

Sharing is caring:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *