Phenny Awiti atarajia mtoto wa tatu bila Virusi Vya Ukimwi

Image may contain: 1 person

Phenny Awiti ambaye ni shujaa wa kupigana na Virusi Vya Ukimwi (VVU) ana furaha wa kukata na shoka baada ya kubeba mimba kwa mara ya tatu.

Awiti alionyesha furaha yake kwenye mtandao wa kijamii akielezea kuwa anatarajia mtoto wa tatu mwenye hana virusi vya ukimwi.

Hii inakuja muda mfupi baada ya mama wa watoto wawili kupewa posa na Mjerumani.

“Kwa hivyo mchumba yangu aliniita sebuleni, nilikuwa bado mvivu kitandani na akasema kwamba ana kitu cha kunionyesha kutoka sebuleni, kwa hivyo ilinibidi nitoke chumbani na kwenda ili nione ni nini,” Awiti alielezea jinsi alivyo pewa posa.

Awiti hajawahi kuwa na aibu kwa kuelezea maisha yake na kuishi na virusi vya ukimwi hata kama imekuwa changamoto kwa namna fulani maishani mwake.

Image may contain: 2 people, people smiling, close-up

Aligundua kuwa alikuwa na virusi akiwa shule ya upili na maisha yake ilibadilika kabisa.

Watoto wake wawili hawana virusi vya ukimwi na amechukua kila hatua kuwatunza na kuwalea wawe na afya nzuri.

Akipelekea kwa mtandao wa kijamii, Awiti alifurahia kuelezea mimba yake ya tatu na matarajio ya kulea mtoto bila virusi.

They say when she is lost, she is pregnant๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜˜ On a journey, to raising another HIV Negative Baby! (Walisema anapopotea, ni mjamzito.. kwenye safari ya kulea mtoto mwingine bila Virusi Vya Ukimwi (VVU)

Awiti amekuwa kilelezo kwa jamii na kukomesha dhana mbaya kwa watu waliougua ukimwi huku akitoa mafundisho kuhusu kutumia tembe na kulea watoto.

https://www.instagram.com/p/B2OCcSEH8EC/?utm_source=ig_web_copy_link

Do you have any information that you would like Daily Buzz to publish or highlight? Get to us on info@dailybuzz.co.ke

Sharing is caring:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *