Wafu wazikwa katika makaburi ya pamoja Morogoro Tanzania

Image result for morogoro fire victims mass grave

Wafu wamezikwa kwa kaburi la pamoja baada ya kukumbana na mkasa wa moto ulioua watu zaidi ya 60.

Mamia ya jamaa na rafiki walikongamana katika uwanja wa shule ya upili ya Morogoro ili kuwatambua wapendwa wao walioathirika katika ajali ya lori la mafuta.

Polisi walisema kuwa watu hao walikuwa wakichota mafuta baada ya lori kupoteza mwelekeo siku ya Jumamosi.

Image result for morogoro fire victims mass grave

Bado chanzo cha ajali hiyo ya kutisha hakijabainika wazi lakini kuna hofu idadi ya watu walioteketea ikaongezeka.

Washahidi wa ajali hiyo walielezea kuwa waendesha pikipiki ndio walioathirika zaidi na mkasa huo.

Miili iliyoteketezwa ilizikwa kwa kaburi la pamoja katika eneo la Morogoro ambapo viongozi wengi walimiminika pamoja na wananchi wa sehemu mbalimbali.

 

Do you have any information that you would like Daily Buzz to publish or highlight? Get to us on info@dailybuzz.co.ke

Sharing is caring:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *